Wakati mkutano wa 19 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukiendelea jijini Dodoma Juni 24, 2025 pamoja na mambo mengine wabunge watapiga kura kupitisha bajeti kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 56.49 kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Bajeti hiyo inajumuisha stahiki za watumishi na michango ya pensheni (Serikali Kuu) shilingi trilioni 9.17 pamoja na ununuzi wa bidhaa na huduma shilingi trilioni 5.58.
Bajeti hiyo inatarajiwa kugharamiwa na mapato ya ndani ya shilingi trilioni 40.47 misaada shilingi trilioni 1.07 na mikopo ya shilingi trilioni 14.95.
Kati ya mapato ya ndani yanayotarajiwa mapato ya kodi ni shilingi trilioni 32.31 mapato yasiyo ya kodi shilingi trilioni 6.48, na mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa shilingi trilioni 1.68.
Aidha mikopo inajumuisha shilingi trilioni 6.27 kutoka vyanzo vya ndani na shilingi trilioni 8.68 kutoka vyanzo vya nje.