Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya Kibaha Mkoa wa Pwani imetoa hukumu ya kifungo cha maisha jela kwa Yasini Hassan Kibabu, Miaka 19, Mkulima na mkazi wa Ungindoni, Kibaha baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka mitatu.
Mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai 14, 2024 katika mtaa wa Mailimoja, Kibaha baada ya kumvizia mtoto huyo akiwa maeneo ya jirani na nyumbani kwao kisha kumkamata na kumuingilia kinyume na maumbile.
Akisoma hukumu hiyo Juni 23, 2025 Mh. Fredrick Shayo ameeleza kuwa Mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka hivyo kumtia hatiani Bw. Yasini Kibabu na hukumu hiyo ni fundisho kwa wengine ambao wana tabia kama hizo.
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii