Tehran yatishia kushambulia nchi yoyote itakayotumiwa na majeshi ya Marekani kuishambulia Iran.

Mshauri wa Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ameahidi kwamba kambi zinazotumiwa na majeshi ya Marekani kufanya mashambulizi dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran, pamoja na nchi zinazoyahifadhi, "zitalengwa na mashambulizi" ya Iran.

Nchi yoyote katika eneo hilo au mahali pengine itakayotumiwa na vikosi vya Marekani kuishambulia Iran itachukuliwa kuwa lengo halali la majeshi yetu," Ali Akbar Velayati amenukuliwa akisema na shirika la habari la serikali la IRNA.

 Marekani "haina nafasi tena" katika kanda na hata kwingineko, "katika ulimwengu wa Kiislamu," ameongeza. "Marekani imeshambulia moyo wa ulimwengu wa Kiislamu na lazima itarajie madhara yasiyoweza kurekebishwa, kwa sababu Jamhuri ya Kiislamu haivumilii matusi au uchokozi wowote dhidi yake." 

Marekani yawarejesha makwao wanadiplomasia wake waliotumwa Iraq

Wafanyakazi wapya katika ubalozi wa Marekani waliondoka Iraq kati ya Jumamosi na Jumapili kama sehemu ya juhudi zinazoendelea za "kuboresha operesheni," afisa wa Marekani ameliambia sirika la habari la AFP. Kuondoka huku ni sehemu ya mchakato ulioanza wiki iliyopita "kutokana na tahadhari nyingi na kutokana na mvutano wa kikanda," chanzo hicho kimesema.

 Hapo awali, ubalozi wa Marekani mjini Beirut uliripoti kwamba Wizara ya Mambo ya Nje iliamuru familia za wafanyakazi na wafanyikazi wasio wa lazima wa serikali ya Marekani kuondoka Lebanon.

IAEA inasema milango ya handaki kwenye kitoo cha Isfahan nchini Iran yashambuliwa

Njia za kuingilia kwenye kito cha nyuklia ca Isfahan nchini Iran zimeshambuliwa jeshi la Marekani jana usiku, Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki limesema. "Tumetambua kwamba milango ya chini ya ardhi kwenye kituo cha Isfahan imelengwa na mashambulizi ya Marekani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran yuko Moscow kwa mazungumzo na Vladimir Putin

Abbas Araghchi, ambaye mwenyewe alitangaza kutoka Istanbul kwamba angesafiri hadi mji mkuu wa Urusi kuonana na Bw. Putin, "amewasili Moscow kwa mashauriano na rais (wa Urusi) na maafisa wengine kuhusu hali ya kikanda na kimataifa kufuatia mashambulizi ya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii