Rais wa Sierra Leone achaguliwa kuwa rais wa ECOWAS

Rais wa Sierra Leone, Julius Maada Bio, amechaguliwa kuwa Rais wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS)  Juni 22, wakati wa mkutano wa kawaida wa wakuu wa nchi uliofanyika Abuja, Nigeria. Anachukua urais wa zamu wa taasisi hii ya kikanda, akimrithi Bola Ahmed Tinubu, Rais wa Nigeria.

Rais wa ECOWAS anayemaliza muda wake, amekiri katika hotuba yake "changamoto kali na za mara kwa mara ambazo zinaendelea kukwamisha matarajio yetu." "Miongoni ma changamoto hizo kwa sasa ni vitisho vya usalama, itikadi kali, na mienendo mingine ya kuvuka mipaka" ambayo inaendelea kupanuka na kushika kasi.

Uchaguzi huu wa rais wa Sierra Leone ni mshangao mkubwa. Kwa hakika, ingawa wasifu wa rais wa Ghana ulikuwa umeangaziwa katika kipindi cha mwisho, Bassirou Diomaye Faye, Rais wa Senegal, ndiye aliyependwa zaidi, hasa kwa sababu ECOWAS, hadi sasa, ilikuwa inaheshimu mzunguko usio rasmi kati ya marais wanaozungumza Kifaransa, wanaozungumza Kiingereza na Kireno.

 Hatimaye, marais wawili kutoka nchi zinazozungumza Kiingereza wamepishana kwenye uongozi wa shirika hili la kikanda, na hivyo kuvunja kanuni hii isiyotamkwa ya kupishana uongozini. Jambo moja ni la hakika: Julius Maada Bio atachukua uongozi wa wa shirika hili ambalo linakumbwa na mgogoro wa zaidi ya miaka hamsini.

Kuelekea kuondoka kwa Mali, Burkina Faso, na Niger

Lakini mkutano huu wa Juni 22, 2025, haukuishia tu kwenye uchaguzi huu. Viongozi wa Afrika Magharibi pia wameamua kuteua mpatanishi kusimamia mchakato wa kujiondoa kwa Mali, Burkina Faso, na Niger-nchi tatu zinazotawaliwa na wanajeshi ambazo zimeunda kambi yao wenyewe:

 Muungano wa Nchi za Sahel (ESA). Mpatanishi atasaidiwa na mawaziri watatu kutoka nchi wanachama. Kujiondoa rasmi kwa nchi hizi tatu sa Sahel katika ECOWAS kumepangwa mwishoni mwa mwezi Julai.

Kwa miezi kadhaa, makundi ya kijihadi yameongeza mashambulizi katika eneo hilo. Nchini Mali, kambi za kijeshi vimelengwa; nchini Burkina Faso, uvamizi umeripotiwa, hata katika miji mikubwa; nchini Niger, wanajeshi wamepata hasara kubwa. Hata Nigeria, nchi mwenyeji wa mkutano huo, imeshuhudia kuongezeka kwa mashambulizi, dhidi ya vijiji na kambi za kijeshi.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii