Mradi wa maji Butimba jijini Mwanza wazinduliwa rasmi leo juni 20

Rais Samia Suluhu Hassan amezindua Mradi wa Maji na kituo cha kutibu maji Butimba jijini Mwanza.

Samia amezindua mradi huo  Juni 20, 2025 ikiwa ni mwendelezo na ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Simiyu na Mwanza iliyoanza Juni 15 na atahitimisha Juni 21, 2025.

Akiwa ziarani mkoani Simiyu Rais Samia alizindua na kulifungua rasmi jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, lililojengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh6.5 bilioni, huku akiahidi neema kwa wakulima wa zao la pamba.

Pia alizindua na kufungua viwanda viwili vya kuongeza thamani ya mazao, kikiwemo kiwanda cha kuchambua pamba na kingine cha kutengeneza mabomba ya maji na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika jitihada za kuboresha na kuimarisha sekta ya kilimo nchini.

Aidha Rais Samia alizindua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji na uchakataji wa zao la pamba cha MOLI Oil Mills kilichopo Bariadi.

Juni 16, 2025 Rais Samia alizindua Shule ya Wasichana ya Mkoa wa Simiyuna kusema kwamba Serikali haitabagua jinsia katika uwekezaji wa elimu ya sayansi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii