Serikali imeshauriwa kuacha kutoza kodi katika sekta ya gesi asilia na matokeo yake waache wawekezaji waingie, huku ikitafuta vyanzo vingine vya mapato kama vile kuongeza ushuru kwenye samaki wanaoingia kutoka nje na kupunguza ushuru wa makaa ya mawe ili upate wateja wengi kutoka nje.
Hayo yamezungumzwa leo Juni 18, 2025 bungeni jijini Dodoma na Mbunge wa Muleba Kaskazini, Dk Charles Mwijage wakati akichangia taarifa ya maoni ya Bajeti Kuu ya Serikali kuhusu hali ya uchumi wa taifa kwa Mwaka 2024, mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka wa Fedha 2025/26 na Makadilio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/26.
Mwijage amesema kuwa gesi asilia ni usalama wa nchi hivyo Serikali isiweke ushuru wowote katika bidhaa hii ila wasaidiane kutafuta vyanzo vingine vya mapato vitakavyoisaidia nchi kuinua uchumi wake lakini siyo kuweka ushuru kwenye sekta hiyo.