Askari polisi wapya 4,800 wasajiliwa PSSSF

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umesajili askari polisi watarajiwa 4,800 wanaokaribia kumaliza mafunzo yao katika Shule ya Polisi Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kabla ya zoezi la usajili maafisa wa PSSSF wakiongozwa na Meneja wa Kanda ya Kati Dodoma Bw. Michael Bujiba walitoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa askari hao wapya.

Akizungumza katika zoezi hilo kwa niaba ya PSSSF Bw. Bujiba alisema zoezi hilo la usajili ni ishara tosha kwamba Mfuko utakuwa pamoja nao katika maisha yao ya utumishi na maisha ya kustaafu.

Leo wanaajiriwa na Serikali wakiwa na nguvu zeo na watalipwa mshahara lakini Serikali kwasababu inawajali inawaandalia maisha yenu ya baada ya utumishi kupitia Mafao ya uzeeni.

Naye Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) wa Jeshi la Polisi Makao Makuu Kitengo cha Fidia na Mafao Bw. Basil Pandisha, ameipongeza PSSSF kwa utoaji elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa askari hao wapya lakini pia hata kwa askari ambao tayari wamesajiliwa

Aidha aliwakumbusha kutambua kuwa wameingia kwenye ajira lakini utafika wakati wa kustaafu hivyo ni vema wakajipanga kuanzia sasa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii