Serikali kuongeza posho kwa wenyeviti wa vijiji kutoka 100,000% hadi laki 300,000%

Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo ameibua hoja nzito kuhusu malipo na maslahi ya wenyeviti wa serikali za mitaa akisema kundi hilo limekuwa likipuuzwa licha ya kuwa nguzo muhimu ya utawala wa karibu na wananchi. 

Akichangia bajeti ya Serikali Kuu bungeni Gambo alisema wenyeviti hao ndio wa kwanza kushughulikia masuala ya msingi kama ukusanyaji wa mapato ya halmashauri na utatuzi wa migogoro ya kijamii.

Kwa mujibu wa Gambo mwenyekiti wa serikali ya mtaa hulipwa posho ya Sh 100,000 kwa mwezi lakini kiasi hicho si tu kwamba ni kidogo bali pia hakilipwi kwa wakati.

Hivyo amebainisha kuwa Wapo baadhi ya wenyeviti katika jiji la Arusha ambao hawajalipwa posho zao tangu mwezi Machi huku akifafanua kwamba akilinganisha hali hiyo na watumishi wa umma wengine kama wabunge na madaktari wanaolipwa kwa wakati na pia kupata kiinua mgongo baada ya muda wao wa utumishi.

Ametoa wito kwa serikali kuongeza posho za wenyeviti hasa katika majiji yenye makusanyo makubwa kama Arusha, Dodoma na Dar es Salaam hadi kufikia angalau Sh 300,000 kwa mwezi. 

Gambo alisema ni muhimu wenyeviti hao kutambuliwa kwa kazi kubwa wanayoifanya na kuepuka kuwafanya kuwa wahanga wa mifumo isiyo na maridhiano ya haki na wajibu

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii