Waliofaulu usaili jeshi la polisi kuripoti juni 12 kwaajili ya kuhudhuria mafunzo.

Jeshi la Polisi Tanzania limewataka vijana waliochaguliwa kujiunga nalo kuripoti katika Shule ya Polisi Moshi kuanzia Juni 12 hadi 14 2025 kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo.

Vijana hao ni wale waliofanya maombi na kufaulu katika usaili uliofanyika katika maeneo mbalimbali nchini.

Taarifa ya wito huo imetolewa jana Jumapili Juni 1, 2025 na Mkuu wa Jeshi la Polisi Camilius Wambura.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo waliofanyiwa usaili Dar es Salaam kwenye vikosi vilivyo chini ya makao makuu ya jeshi hilo wataripoti jijini humo katika uwanja wa gwaride uliopo Kambi ya Polisi barabara ya Kilwa.

Ikiwa Vijana hao kutokana na taarifa hiyo inaelezwa kuwa wanatakiwa kuripoti Juni 12, 2025 saa 12.00 asubuhi kwa ajili ya safari ya kwenda Shule ya Polisi Moshi.

Kwa upande wa waliofanyiwa usaili katika mikoa ya Tanzania Bara wanatakiwa kuripoti kwa makamanda wa polisi wa mikoa waliofanyia usaili, Juni 11, 2025 saa 2.00 asubuhi kwa ajili ya kupewa utaratibu wa safari ya kwenda Moshi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii