Mkutano mkuu wa SADC kuhamasisha utalii nchini Tanzania

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda amefungua rasmi Mkutano wa 33 wa mwaka wa Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika jijini Arusha.

Akizungumza leo Ijumaa Mei 30, 2025 wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Makonda amewakaribisha wakuu hao wa majeshi kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Mkoa wa Arusha huku akiwahimiza kutumia fursa ya kuwepo mkoani humo kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo Arusha na mikoa jirani.

Makonda amesema kuwa ikiwa tanzania tuna vivutio vingi vya utalii vinavyopatikana katika mkoa huu na mikoa jirani kama vile Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Arusha National Park, Mbuga ya Wanyama Tarangire, Mlima Kilimanjaro pamoja na Mbuga ya Wanyama Serengeti hivyo amewataka kutumie fursa hiyo muhimu.

Mkutano huo unaoongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Jacob Mkunda, ulianza Mei 26, na unatarajiwa kuhitimishwa kesho Mei 31, 2025.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii