Wafungwa watano wameuawa Ivory Coast

Wafungwa watano wameuawa katika gereza nchini Ivory Coast wakati wa msako ambao ulibadilika na kuwa makabiliano baina ya maafisa na wafungwa, mwendesha mashtaka wa umma amesema.

Taarifa ya mwendesha mashtaka Abel Nangbele Yeo imeongeza kwamba zoezi hilo lilikumbana na upinzani kutoka kwa wafungwa na kwamba jumla ya watu 29 wamejeruhiwa katika gereza la katikati mwa jiji la Bouake na ambapo kati yao ni maafisa sita na wafungwa 23.

Baada ya maafisa kuzidiwa ndipo walifyatua risasi za onyo ili kudhibiti vurugu na kurejesha utulivu.

Umoja wa Mataifa umeeleza wasiwasi wake kuhusu ripoti za "msongamano mkubwa wa wafungwa" na hali mbaya ya magereza nchini Ivory Coast huku mashirika ya kiraia ya nchini humo pia yakionya kuhusu utitiri wa wafungwa magerezani ambao kesi zao hazijapekwa mahakamani.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii