Yuko wapi kiongozi wa upinzani Matata Ponyo, Waziri Mkuu wa zamani na mbunge wa kitaifa? Akiwa amehukumiwa tangu Mei 20 hadi miaka 10 ya kazi ya kulazimishwa na Mahakama ya Kikatiba kwa ubadhirifu wa fedha za umma akiwa madarakani, mwanasiasa huyo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ametoweka, kwa mujibu wa chama chake cha kisiasa.
Matata Ponyo hapatikani tena kwa simu wala nyumbani kwake hayupo. Waziri Mkuu huyo wa zamani wa DRC alikuwa Kinshasa mwishoni mwa juma hili lililopita. Franklin Tshiamala, katibu mkuu wa chama chake cha siasa LGD, anaelezea wasiwasi wake. "Tulijaribu kutembelea magereza ambako pengine angeweza kuwa. Hayupo. Tuliamua kutoa tahadhari hii kuiomba serikali itueleze alipo." Tunawasiliana na familia yake, ambayo pia ina wasiwasi. Tunaogopa kuwa huenda aliuawa. Tunataka kujua alipo. Ingetutosha kama mamlaka, ambayo iko katika nafasi nzuri zaidi, ingeweza kutuambia Matata Ponyo yuko wapi sasa hivi."
Mjumbe wa serikali ya DRC na afisa mmoja, waliowasiliana na RFI jioni ya Mei 31, amewaelezea viongozi wa chama cha Matata kama "wacheshi" au hata "waigizaji," akimaanisha kuwa wanasiasa hao wafahamu kuwa kiongozi wao alitoroka kisiri kutoka Kinshasa. Franklin Tshiamala almejibu. "Baadhi wamesema yuko Marekani, wengine hata wamedai yuko Ubelgiji, na wengine Ufaransa. Kauli au ujumbe wa Twitter kutoka kwa afisa mkuu wa kisiasa nchini humo zimedai kuwa anaonekana yuko nchini na kwamba atakamatwa hivi karibuni. Tuliona picha hizi kwenye mitumbwi na picha zingine kwenye magereza." Katika haya yote, ninaingilia kati kwa sababu hapatikani."
Wakati huohuo, chama cha Matata Ponyo kinadai kuwa bintiye, ambaye alitaka kusafiri kwenda Marekani, alipigwa marufuku kuondoka kwenye ardhi ya Kongo, pasi yake ya kusafiria ikichukuliwa na mamlaka ya uhamiaji.