EID EL-ADH’HAA KUANGUKIA SIKU YA JUMAMOSI JUNE 7

Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) limetoa taarifa kwa Waislamu na Wananchi wote kwa jumla kuwa Sikukuu ya Eid El-Adh’haa itakuwa siku ya Jumamosi June 07, 2025.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa BAKWATA Alhaj Nuhu Jabiri Mruma imesema sherehe za Eid El-Adh’ha kitaifa kwa mwaka huu zitafanyika Mkoa wa Dar es salaam na Swala ya Eid itaswaliwa katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI BAKWATA Makao Makuu Kinondoni kuanzia saa 1.30 asubuhi na kufuatiwa na Baraza la Eid mara tu baada ya Swala.

Katika hatua nyingine Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar imetangaza kuwa Sikukuu ya Eid Al-Adha itakuwa siku ya Jumamosi  June 07,2025 sawa na Mwezi 10 dhul-hijjah 1446H ambapo Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume amesema swala na Baraza la Eid el Adh-haa mwaka huu vitafanyika Wilaya ya Kati ambapo swala itasaliwa katika Msikiti wa Ijumaa Bambi saa 1:15 asubuhi na Baraza la Eid litafanyika katika Viwanja vya Skuli ya Suza Tunguu Unguja.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii