Watu 35 mbaloni kwa uuzaji wa mafuta ya dizeli na petroli kiholela.

Watu 35 wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Mwanza kwa tuhumza za kufanya biashara ya kuuza mafuta ya dizeli na petroli bila kuwa na kibali na kuyahifadhi katika makazi yao bila kufuata taratibu pamoja na kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi.

Katika tukio la usafirishaji wa bangi kamanda Mutafungwa amesema tarehe 30 May, 2025 majira ya saa tatu usiku katika kitongoji cha Iseni wilayani Magu walikamatwa watu wawili Jeny Odhiambo na Samora Nyandimo walikamatwa wakiwa wanasafirisha bangi kilogramu 194 walikuwa wakitoka nayo Tarime mkoani Mara kuja Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa Habari kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza DCP Wilbrod Mutafungwa amesema watu hao wamekamatwa katika kata za Koromoje, Ngula, Ilemela, Nyshishi, Buhongwa kupitia msako maalum ulioanza April 30 hadi May 31 mwaka huu.

Kamanda Mutafungwa amesema watuhumiwa hao wamekutwa na mafuta ya dizeli lita 685, betri mbili za magari, pikipiki moja, mapipa mawili mipira kumi ya kunyonyea mafuta, madumu 85 pamoja na vitu vingine vyenye thamani ya shilingi milioni nne

Ili kupata taarifa zaidi endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya www.jembenijembe.com kupitia Instagram ,Facebook, tikok,x zamani twitter pamoja na YouTube 



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii