Ongezeko la Wakezaji kutoka njee ya nchi wana tabia ya kukwepa kodi

Mbunge wa Sumve Kasalali Mageni ameibua hoja kuhusu ongezeko la wafanyabiashara kutoka mataifa ya Asia hususan China akisema kuwa pamoja na wingi wao wamekuwa na tabia ya kukwepa kodi.

Mageni amezungumza hayo wakati akichangia makadirio ya bajeti ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2025/2026 amesema kuwa baadhi wafanyabiashara wa kigeni pamoja na wale wa ndani wamekuwa na tabia ya kukwepa kutumia mifumo ya kielektroniki ya malipo na badala yake wanapendelea kufanya miamala kwa njia ya fedha taslimu (cash) ili kukwepa kodi.

Aidha mbunge huyo ameitaka serikali kuimarisha udhibiti wa mifumo ya ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha kuwa mifumo ya kielektroniki inatumika kikamilifu kwa wafanyabiashara wote bila ubaguzi ili kuongeza mapato ya ndani na kulinda uchumi wa taif

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii