Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan, akizuru Kyiv, amependekeza siku ya Ijumaa kuwa Uturuki iandae mkutano kati ya Rais wa Urusi Vladimir Putin, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, na Rais wa Marekani Donald Trump.
"Tunaamini kwa dhati kwamba inawezekana kuhitimisha mazungumzo ya kwanza na ya pili ya Istanbul kwa mkutano kati ya Bw. Trump, Bw. Putin, na Bw. Zelensky, chini ya uongozi wa (Rais wa Uturuki) Erdogan," Fidan amesema katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na mwenzake wa Ukraine Andriy Sybiga.
"Tunaweza kufumbia macho kuendelea kwa vita hivi au kupata amani ya kudumu ifikapo mwisho wa mwaka," waziri wa mambo ya nje wa Uturuki ameongeza, akisema "matarajio ya kusitishwa kwa mapigano na amani yameongezeka."
"Hakika maendeleo yanaweza kupatikana mradi tu tubaki kwenye meza ya mazungumzo," amesema Bw. Fidan, ambaye anatarajiwa kupokelewa siku ya Ijumaa na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.