Mahakama ya Tanzania imetangaza kuwa kesi mbili za jinai namba 8606/2025 na 8607/2025 kati ya Jamhuri na Tundu Antiphas Lissu zitatajwa na kusikilizwa leo Jumatatu Juni 2 mubashara katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi lengo la kurusha matangazo hayo moja kwa moja ni kuwawezesha wananchi kufuatilia mashauri bila ulazima wa kufika mahakamani. Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama unaolenga kuimarisha uwazi, uwajibikaji, na matumizi ya teknolojia katika utoaji haki.
Mahakama imeeleza kuwa ukumbi una uwezo wa kuchukua watu 80 pekee. Nafasi zimetengwa kwa mawakili wa Serikali, utetezi, waandishi wa habari, na watu wachache waliobainishwa.
Ili kupata taarifa zaidi endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya www.jembenijembe.com kupitia Instagram ,Facebook, tikok,x zamani twitter pamoja na YouTube