TUME YA MAADILI YA UONGOZI WA UMMA YAOMBA USHIRIKIANO BAINA YA VIONGOZI

TUME ya Maadili ya Viongozi wa Umma imewataka wahariri na waandishi wa habari kuendelea kushirikiana nayo katika kuwaibua viongozi wanaokiuka maadili ili kuimarisha uwajibikaji na utawala bora nchini.

Akizungumza  Mei 30, 2025 katika kikao cha wahariri kilichoandaliwa na Sekretarieti ya Maadili, Kamishna wa Maadili, Jaji Sivangilwa Mwangesi, amesema malalamiko mengi kutoka kwa wananchi yamekuwa yakihusisha matumizi mabaya ya madaraka na ukiukwaji wa maadili na hivyo Tume imeanzisha mfumo rasmi wa kupokea malalamiko kutoka kwa umma.

Aidha amefafanua kuwa majukumu ya Tume ni kupokea na kuchunguza malalamiko dhidi ya viongozi wanaokiuka maadili ya wananchi huku wakihimizwa kuripoti viongozi wanaotumia madaraka yao vibaya kwa kutumia mifumo rasmi ya Sekretarieti.

Ameongeza kuwa tume imeandaa semina kwa wahariri na waandishi wa habari ili kuwajengea uwezo wa kuelimisha jamii kuhusu maadili ya viongozi wa umma.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii