ZIARA YA MAJALIWA YA.KUTANISHA NA WAZIRI WA JAPAN

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na Waziri Mkuu wa Japan Ishiba  Shigeru ambaye amemuhakikishia kuwa nchi hiyo itaendelea kuimarisha ushirikiano na Tanzania jambo ambalo linalenga kuchochea ukuaji wa uchumi kutokana na fursa zitakazoendelea kupatikana kupitia mahusiano hayo.

Amekutana na kiongozi huyo  May 29, 2025 katika ofisi ya Waziri Mkuu Tokyo Japan ambapo PM Majaliwa amesema ahadi hiyo inazidi kutoa fursa ya Wawekezaji na Wafanyabiashara wa Japan pamoja na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) kuendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Japan amepongeza kuendelea kuimarika kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Japan na kwamba ameahidi kuhakikisha makampuni mbalimbali ya Japan yataendelea kufanyakazi na Tanzania ili kuisaidia katika kukuza uchumi, kuendelea masuala ya kijamii na teknolojia kwani wanatambua idadi ya watu nchini inaendelea kuongezeka.

PM Majaliwa ametumia fursa hiyo kumueleza Waziri Mkuu huyo kuwa  pamoja na miradi mingine wanayotekeleza nchini Japan kupitia JICA iangalie uwezekano wa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuzifanyia ukarabati mkubwa barabara za Morogoro-Dodoma na barabara ya Kibiti-Lindi ambayo imeharibika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii