Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kinatarajia kuanza ziara rasmi kuanzia tarehe 3 Juni mwaka huu katika jiji la Mwanza.
Ziara hiyo inalenga kuwakaribisha wanachama wapya, kutambulisha safu ya uongozi wa chama pamoja na kutangaza tarehe rasmi ya uzinduzi wa shughuli zake.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza, Naibu Katibu Mkuu wa CHAUMMA Tanzania Bara, Benson Kigaila, amesema kuwa ziara hiyo itaanzia jijini Mwanza na kuendelea katika mikoa yote ya Tanzania Bara.
"Tunatarajia kumaliza ziara yetu tarehe 16 Juni katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha," alisema Kigaila.
Kigaila amesisitiza kuwa ziara hii ni sehemu ya mikakati ya chama hicho kujiimarisha kitaifa na kuwasiliana moja kwa moja na wananchi kuhusu dira na malengo ya CHAUMMA..