Maelfu ya watu wenye njaa kali wamevamia ghala la misaada katikati mwa Ukanda wa Gaza tukio lililoshuhudiwa kupitia shirika la habari la Reuters. Katika vurugu hizo milio ya risasi ilisika huku watu wakisukumana kuingia na kuchukua chakula.
Kwa mujibu wa madaktari wa Hospitali ya al-Aqsa, watu wanne walipoteza maisha na wawili kukanyagwa katika msongamano na wawili kwa kupigwa risasi, ingawa bado haijajulikana waliowafyatulia risasi ni kina nani.
Tukio hili limetokea wakati hali ya kibinadamu Gaza ikizidi kudorora na Umoja wa Mataifa ukionya kuhusu tishio la baa la njaa linalowakabili maelfu ikumbukwe kuwa Siku moja kabla ya tukio hilo jeshi la Israel ilifyatua risasi za onyo karibu na kituo cha misaada cha GHF kilichokuwa kimevamiwa na raia waliokuwa wakisubiri msaada.