WAJUMBE WA KAMATI KUU CCM WAPEWA JUKUMU LA KUISAMBAZA ILANI YA CHAMA UCHAGUZI UTAKAPOWADIA

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefungua mkutano mkuu wa CCM unaofanyika Dodoma na kueleza kuwa agenda kubwa itakuwa ni kuipitia ilani ya uchaguzi mkuu ya chama hicho na kuiweka hadharani Ilani yake mpya ya 2025-2030 ambayo itanadiwa wakati wa Uchaguzi Mkuu 2025.

Amesema hayo leo  Mei 29, 2025, wakati akifungua Mkutano Mkuu wa CCM unaofanyika kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, ambapo amesema ilani hiyo imeandaliwa kwa weledi mkubwa na imewashirikisha wadau mbalimbali na  imesheheni mambo mazuri kwa maendeleo ya Watanzania.

Hivyo ameongeza kuwa matarajio yake ni kuona wajumbe wa mkutano huo wakibeba jukumu la kuisambaza ilani hiyo kwa wananchi pale wakati utakapowadia  rasmi wa kampeni.

Awali katika mkutano baadhi ya viongozi kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), London Diaspora wamewasili nchini Tanzania kwajili ya kushiriki Mkutano Mkuu wa CCM unaofanyika Dodoma ikiwa Wanachama hao wameongozwa na mkuu wa msafara, Allynotty Mustafa , Elizabeth Kabale, Beatrice Bategereza, Rhodah Mwanga na Haruna Mbeyu huku wakiunga  mkono juhudi zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii