WABUNGE WAHIMIZWA KUFUATA KANUNU NA SHERIA ZA BUNGE

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Tulia Ackson ametoa onyo kali kwa wabunge akiwataka kuzingatia matakwa ya Katiba, sheria na kanuni za Bunge wakati wa kujadili hoja mbalimbali kwa kusisitiza umuhimu wa kulinda heshima na hadhi ya chombo hicho cha kutunga sheria.

Akizungumza leo Mei 28, 2025 bungeni jijini Dodoma wakati wa kuahirisha shughuli za Bunge Dk Tulia amesema baadhi ya michango iliyotolewa wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu uliofanyika Mei 26 na 27, 2025 iliashiria ukiukwaji wa masharti ya Kanuni ya 71 ya Kanuni za Bunge.

Ameeleza kuwa utaratibu wa Bunge upo wazi na unaweka mipaka ya namna mijadala inavyopaswa kufanyika kwa uhuru wa kutoa maoni  hivyo haupaswi kugeuzwa kuwa kisingizio cha kutoa kauli au mitazamo inayokiuka kanuni au kuashiria misimamo isiyo rasmi ya Bunge.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii