Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameendelea na ziara yake Toyko nchini Japan kwa kuwashawishi Wawekezaji na Wafanyabiashara wakubwa wa Japan kuja kuwekeza kwenye sekta ya kilimo, afya, uchumi wa buluu, nishati, pamoja na miundombinu ya ufugaji wa TEHAMA kwani Serikali imekwisha boresha mazingira rafiki kwa ufanyaji biashara na uwekezaji.
Ameyasema hayo leo May 28, 2025 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokutana na Viongozi wa Shirikisho la Wawekezaji katika Sekta za Miundombinu, Shirikisho la Wawekezaji na Wafanyabiashara nchini Japan (KEIDANREN) na Jumuiya ya Wamiliki, Marais na Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Makampuni za Japan (KEIZA DOYUKAI) .
Aidha Mei 27, 2025 Majaliwa alikutana na Naibu Waziri wa Ardhi Miundombinu na Usafirishaji Utalii wa Japan (MLIT), Kenichi Ogasawara pamoja na Rais wa Shirikisho la Wawekezaji katika Sekta za Miundombinu Japan na Afrika (JAIDA) Miyamoto Yaichi.