Rais William Ruto ameomba msamaha kwa vijana na mataifa jirani waTanzania na Uganda katika hatua inayotafasiriwa kuwa ilitokana na malumbano makubwa ambayo yamedumu mitandaoni kwa wiki mbili sasa kufuatia kisa kilichoanza na kurushwa kwa kinara wa PLP Martha Karua.
Bi. Karua, pamoja na wanaharakati wengine wakijumuisha Jaji Mkuu wa zamani Willy Mutunga walizuiwa kuingia nchini Tanzania kuhudhuria kusikilizwa kwa kesi ya uhaini ya Kiongozi wa Chadema Tundu Lissu.
Ametoa lai hiyo leo Mei 28, 2025 wakati wa hotuba yake kwa taifa katika hafla ya Maombi ya Kitaifa ambayo kuwakutanisha na kuwaleta pamoja viongozi wa serikali Rais Ruto amesema ikiwa kuna jinsi viongozi wamewaendea visivyo vijana wa Gen Z, basi anaomba radhi.