DKt, SAMIA AMEZINDUA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI LA MAKAO MAKUU DODOMA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Mei 28, 2025, ameweka jiwe la msingi la jengo jipya la Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jijini Dodoma akisema tukio hilo ni la kihistoria na linaakisi ndoto ya waasisi wa chama hicho wakiongozwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Aidha amesisitiza kuwa jengo hilo litakapokamilika halitakuwa tu ofisi ya utawala, bali pia alama ya kudumu ya umoja uimara na utambulisho wa CCM ndani na nje ya nchi.

Rais Samia amesema jengo hilo ni mwelekeo wa CCM kuelekea siku zijazo likiwa sehemu ya utekelezaji wa ndoto kubwa za maendeleo utawala bora na usimamizi imara wa chama katika mazingira ya kisasa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii