SHEIKH WA MKOA WA MWANZA HASSAN KABEKE AMEELEZA ITAKAPOFIKA JUNE 12 2025 ITAFANYIKA DUA MAALAMU YA KULIOMBEA TAIFA NA MUOMBEA RAIS MHE DR SAMIA SULUHU HASAN KATIKA ENEO LA GANDH HALL JIJINI MWANZA.
AMESEMA LENGO LA DUA HIYO NI KUMTIA MOYO MHE RAIS KATIKA MAJUKUMU YAKE NA KUENDELEA KUSIMAMIA SHERIA ZA NCHI BILA HOFU YOYOTE.
SHEIKH KABEKE AMEYASEMA HAYO AKIZUNGUMZA NA WAAANDISHI WA HABARI KATIKA OFISI ZA BAKWATA MKOA WA MWANZA.
AIDHA SHEIKH KABEKE AMEONGEZA KUWA BAKWATA MKOA WA MWANZA WANATEKELEZA AGIZO LA MUFTI WA TANZANIA SHEIKH ABUBAKAR ZUBER BIN ALI AMEWATAKA WAISLAMU NCHINI KUMSOMEA DUA MHE RAIS
CHANZO ;JEMBE HABARI