Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Serikali haitavumilia baadhi ya mashirika ya umma kuendelea kunufaika kwa kutumia rasilimali za umma bila kurejesha faida inayostahili kwa Serikali.
Akizungumza leo Juni 10, 2025 katika hafla ya upokeaji wa gawio na michango kutoka kwa mashirika ya umma iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Samia amesema alisisitiza kuwa zama zile za mashirika kuchuma serikalini bila kurudisha faida zimepitwa na wakati na hazipo tena na kuyataka mashirika yajibebe na yaibebe Serikali pia yawe walinzi wa uwekezaji uliofanywa na Serikali kwa kuilinda miundombinu ya uwekezaji, isiwe chanzo cha tutakosa faida.
Ameongeza kuwa mashirika yanapaswa kuwa sehemu ya mabadiliko ya kiuchumi kwa kuhakikisha yanaongeza ufanisi, uwajibikaji, na kuleta tija kwa wananchi kupitia michango ya mapato kwa Serikali.