Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linasema watu milioni 13 kote katika Pembe ya Afrika wanakabiliwa na njaa kali kutokana na kuendelea kwa ukame.
Mavuno yaliyoshindikana na uhaba wa chakula unalazimisha familia kutoka makwao, WFP inasema, na msaada wa haraka unahitajika ili kuzuia mzozo wa kibinadamu.
Msimu wa mvua umekosa kutokea kwa miaka mitatu mfululizo - na ukame unaendelea.
Mazao yamevurugwa, mifugo inakufa, na watu milioni 13 nchini Ethiopia, Somalia, na Kenya wana njaa.
Bei ya vyakula inapanda, na kutokana na mavuno adimu , mahitaji ya wafanyakazi wa kilimo yanapungua, na hivyo kuongeza shinikizo kwa familia zinazojaribu kujilisha.
Bila msaada wa haraka, WFP inasema, janga la kibinadamu haliwezi kuepukika.
WFP inaomba $327m (£242m) kukabiliana na ukame - katika muda mfupi ili kutoa chakula na ruzuku ya fedha, na katika muda mrefu kujenga uwezo wa kustahimili wa jamii za wakulima ambapo mvua kidogo na ukame zaidi unaweza kuwa hali ya kawaida kwa ajili ya mabadiliko ya hali ya hewa