Israel na Hamas wa Palestina Wakubaliana kusitisha mapigano Gaza

Israel na wapiganaji wa Hamas wa Palestina, wamekubaliana kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza, baada ya miezi 15 ya vita kati yao, chini ya usuluhishi wa Marekani na Qatar.

Waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdul Rahman Al Thani amesema makubaliano hayo yataanza rasmi kutekeleza Jumapili ya wiki hii baada ya kuidhinishwa na Baraza la Usalama la Israel.

Rais wa Marekai, Joe Biden amesema kufikiwa kwa makubaliano hayo, kutasitisha mapigano kati ya pande hizo mbili na kutoa nafasi ya misaada ya kibinadamu kuwafikia waathirika wa mapigano hayo na familia kuungana upya.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema nchi yake ipo kwenye hatua za mwisho za kuridhia makubaliano hayo na kumshukuru Rais Biden kwa kuhakikisha makubaliano hayo yamefikiwa.

Kiongozi wa Hamas, Khalil al-Hayya amesema makubaliano hayo yamefikiwa kutokana na uimara wa Wapalestina.

Mamia ya Wapalestina na Waisrael wameupokea uamuzi huo kwa furaha kubwa kwa sababu sasa wanaamini maisha yatarudi kuwa kama yalivyokuwa mwanzo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii