Barabara ya Kenyata Mkuyni Yafunguliwa Baada ya Marekebisho

Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Mwanza, Eng. Ambrose Paschal, amethibitisha kufunguliwa kwa kipande cha barabara ya Kenyata kilichopo Mkuyni, hatua inayopunguza adha kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Eng. Ambrose amesema kuwa barabara hii ilifungwa takribani kwa mwaka mmoja ili kufanyiwa marekebisho ya daraja la Mkuyni, ambalo lilikuwa likihatarisha maisha ya wakazi pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa mita 500, hasa katika kipindi cha mvua.

Ufungaji wa barabara umefanyika kwa kipande kimoja huku shughuli za ujenzi zikiriendelea katika sehemu nyingine. 

Hata hivyo mewaomba wananchi kuwa makini katika kutumia barabara na miundombinu yake ili kuhakikisha usalama wao na uendelevu wa barabara hiyo.

Kwa taarifa zaidi tufuatilie na usikilize jembe Habari Kamili hapo saa kumi kamili alasiri ambapo msomaji wetu wa hii leo ni Gloria Kiwia tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa.

Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii