Serikali imesisitiza kuwa magereza nchini si sehemu ya mateso, bali ni vituo vya marekebisho na maendeleo ya wafungwa kupitia elimu na mafunzo mbalimbali wanapokuwa ndani ya vifungo vyao.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Patrobas Katambi, jijini Dodoma, akibainisha kuwa ushahidi wa mageuzi hayo unaonekana kupitia idadi kubwa ya wafungwa wanaohitimu masomo na kupata stadi za kujitegemea.
Mhe. Katambi amesema wafungwa 209 wamehitimu mafunzo ya ujasiriamali katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), huku wengine 201 wakipata vyeti vya ufundi stadi kutoka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).
Ameeleza kuwa lengo la Serikali ni kuwajenga wafungwa kielimu, kiakili na kiuchumi ili wanaporejea kwenye jamii wawe raia wanaojitegemea na kuchangia maendeleo ya Taifa badala ya kurudia uhalifu.
Aidha, Waziri Katambi amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya magereza kwa kuongeza programu za elimu, mafunzo ya kazi na urekebishaji tabia, ili kulifanya jeshi la magereza kuwa taasisi ya haki na marekebisho, si adhabu pekee.
Kwa taarifa zaidi tufuatilie na usikilize jembe Habari Kamili hapo saa kumi kamili alasiri ambapo msomaji wetu wa hii leo ni Gloria Kiwia tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa.
Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime