Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura, amewataka Watanzania wote kushiriki kikamilifu katika udhibiti na usimamizi wa silaha, hatua inayolenga kuilinda nchi na kutekeleza Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kauli hiyo imetolewa Februari 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam, wakati akizindua rasmi Kamati ya Udhibiti na Usimamizi wa Silaha na kufungua kikao cha kwanza cha kamati hiyo, ambacho kitadumu kwa siku tatu.
IGP Wambura amesema kuwa kikao hicho kitahusisha mafunzo mbalimbali kwa wajumbe wa kamati ili kuimarisha uelewa wao kuhusu majukumu, sheria, kanuni, pamoja na itifaki za kikanda na kimataifa zinazowaongoza katika jukumu la kudhibiti na kusimamia silaha na risasi nchini.
Hata hivyo amesisitiza kuwa ushirikiano wa wananchi ni muhimu ili kuhakikisha usalama wa raia na kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyohusiana na silaha zisizo halali.
Kwa taarifa zaidi tufuatilie na usikilize jembe Habari Kamili hapo saa kumi kamili alasiri ambapo msomaji wetu wa hii leo ni Gloria Kiwia tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa.
Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime