Carter alipokula kiapo cha kuwa rais wa Marekani Januari 20, 1977, aliahidi “serikali nzuri kama watu wake.”
Aliongoza kwa miaka minne yenye misukosuko. Kupanda kwa mfumuko wa bei na kuongezeka kwa ukosefu wa ajira kuliharibu vipaumbele vya ndani vya utawala wake.
Alifanya vyema katika sera za kigeni kwa makubaliano ya amani kati ya Misri na Israeli na mkataba wa Mfereji wa Panama.
Hata hivyo, mgogoro wa mateka nchini Iran ulitawala miaka yake ya mwisho ya White House na kuchangia kushindwa kwake katika uchaguzi mkuu wa 1980.
Lakini Carter alipenda kusema mwisho wa urais wake mwaka 1981 ulikuwa mwanzo wa maisha mapya, akisafiri duniani “kupambana na magonjwa, kujenga matumaini, na kukuza amani.
” Juhudi zake mbalimbali baada ya urais zilimfanua ashinde tuzo ya Amani ya Nobel, 2002.