Kikosi kipya cha kulinda amani nchini Somalia kinachukua nafasi ya ATMIS

Nchini Somalia kikosi kipya cha kulinda amani na kupambana na kundi la kigaidi la Al-Shabaab, kinaanza kazi kuchukua nafasi ya kikosi cha mpito cha Umoja wa Afrika ATMIS.

Kikosi kipya sasa kinafahamika kama A-U-SOM, ambacho kiliidhinishwa mwezi Desemba mwaka uliopita na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mbali na majukumu ya kulinda amani na kupambana na Al-Shabaab, kikosi hiki kipya kina kazi ya kusaidia kurejesha uthabiti nchini Somalia.

Hiki ni kikosi cha tatu cha kulinda amani kutumwa nchini Somalia katika kipindi cha miaka 17 kusaidia kupambana na ugaidi katika nchi hiyo ya pembe ya Afrika.

Kikosi cha A-U-SOM, kina wanajeshi 11,000 ambapo Ethiopia na Burundi, hawashiriki, lakini pia haijafahamika vyema iwapo Kenya na Uganda imetuma wanajeshi wake, lakini Misri ni nchi mpya iliyojiunga katika kikosi hicho.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii