Makaribisho ya mwaka mpya 2025

Miji mikuu kote duniani inajitayarisha kwa sherehe za mwaka mpya baada ya kuaga mwaka 2024 uliogubikwa na vita na msukosuko wa kisiasa.

Nchi zilizo kusini mwa Pacific zitakuwa za kwanza kuukaribisha mwaka 2025.

New Zealand itakuwa ya kwanza kuukaribisha mwaka 2025, saa 18 mbele ya New York, Marekani.

Australia inafuata saa mbili baadae, ambako watu milioni 1 wanatarajiwa mjini Sydney huku milioni mbili wakitarajiwa kuhudhuria sherehe za kukaribisha mwaka mpya katika ufukwe wa Bahari wa Copacabana, nchini Brazil.

Sherehe zimepunguzwa Korea Kusini kutokana na ajali ya ndege iliyotokea Jumapili watu wakiwa katika kipindi cha maombolezi ya kitaifa.

Na nchini Uingereza, hali mbaya ya hewa hasa baridi kali inatishia kuvuruga sherehe za mwaka mpya 2025.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii