Rais Tshisekedi akutana na waathiriwa wa mafuriko jijini Kinshasa

Wakaazi wa jiji la Kinshasa nchini DRC waliojawa na hasira, hapo jana walionesha gadhabu zao kwa Rais Felix Tshisekedi, ambaye alitembelea maeneo yaliyoathiriwa pakubwa na mafuriko ya mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo watu takriban 33 walipoteza maisha.

Wakazi hao walimzomea rais Tshisekedi aliyekuwa ameongozana na mkewe Denis Nyakeru, wakimlaumu kwa kuwaacha bila msaada wowote.

Wakimwita baba,wananachi hao, wengi wakilazimika kufanya uwanja wa michezo wa Kinshasa ,kuwa makazi yao ya muda, walimkabili rais na maswali kuhusu utepetevu katika ujenzi wa miundombinu ya usafiri na usafi jijini Kinshasa.

Mwishoni mwa wiki mto Kongo ulivunja kingo zake baada ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha mafuriko yaliyofunika barabara kuu ya kwenda kwenye uwanja wa ndege, madaraja na vivukio.

Serikali kupitia wizara ya afya na ile ya usalama wa ndani, imethibitisha kuwa familia Zaidi ya elfu tano zimeathirika na watu 50 wamelazwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii