Kulingana na vyanzo kutoka kwenye mkutano kati ya wawili hao, walizungumza kwa karibu saa mbili ambapo DRC ilielezea matumaini yake kwa rais Gnassingbé kwa nafasi yake na kwamba ina imani atasaidia kupatikana kwa suluhu.
Ziara ya rais wa Togo jijini Kinshasa imefanyika baada ya mwezi uliopita nchi ya Qatar sawa na mataifa wanachama wa EAC na SADC kuonekana kuendeleza juhudi katika upatakanaji wa suluhu ya mzozo kati ya DRC na Rwanda.
Wakati viongozi kutoka mataifa ya SADC na EAC wakiwateua wapatanishi wake katika mzozo huo, Doha ambayo ilifanikiwa kuwakutanisha rais Paul Kagame na Tshisekedi, inaongoza pia mazungumzo kati ya M23 na serikali ya Kinshasa.
Kabla ya kwenda Kinshasa, rais Gnassingbe alikutana na mtangulizi wake rais João Lourenço, jijini Luanda.