Shughuli ya kumuaga nguli wa tasnia ya habari Afrika na duniani, Shaka Ssali inatarajiwa kufanyika leo, April 10, 2025.
Shaka, mzaliwa wa Kabale, Uganda alikuwa akifanya kazi kwa muda mrefu katika Shirika la Habari la Voice of America.
Shaka alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 71, Machi 27, 2025 Virginia nchini Marekani.
Enzi za uhai wake, Shaka alijipatia umaarufu mkubwa kupitia Kipindi cha Straight Talk Africa kilichokuwa kikirushwa na VOA.