Rais wa zamani wa Marekani, Jimmy Carter, aliyefariki dunia Jumapili akiwa na umri wa miaka 100, atazikwa tarehe 9 Januari 2025.
Mazishi ya kitaifa yatafanyika katika Kanisa Kuu la Katoliki mjini Washington, D.C., ambapo Rais Joe Biden ameagiza siku hiyo kuwa ya kitaifa ya maombolezo.
Ibada ya kumuaga Carter itaanza Jumamosi, ikijumuisha msafara wa mwili wake kupitia mji aliozaliwa wa Plains, Georgia, na kusimama kwenye shamba alikokulia.
Baada ya hapo, mwili wake utasafirishwa hadi Atlanta na kulazwa katika Kituo cha Carter hadi asubuhi ya Januari 7, kisha kupelekwa Washington, D.C. kwa ibada ya kitaifa.
Carter atazikwa Georgia Januari 9 pembeni ya mke wake, Rosalynn Carter, nyumbani kwao mjini Plains.