Kindiki aapishwa rasmi kuwa Naibu Rais

Aliyekuwa Waziri wa Usalama wa ndani, Prof. Kithure Kindiki ameapishwa rasmi kuwa Naibu Rais mpya wa Kenya, akichukua nafasi ya Rigathi Gachagua ambaye aliondolewa madarakani, huku akiapa kuwa mtiifu kwa rais na kumshukuru Willim Ruto kwa kumuamini.

Akihutubia katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (KICC) jijini Nairobi hi leo muda mfupi baada ya kuapishwa, Prof. Kindiki amesema atahudumu nafasi hiyo kwaa kumsaidia Rais kuongoza Taifa la Kenya na kuwashukuru wale wote waliochangia mafanikio yake.

Amesema, “ninakuahidi Mheshimiwa Rais kuwa nitahudumu chini yako na kukuunga mkono kuiongoza nchi hii. Ninawaahidi katika mkutano huu mbele ya Mungu kwamba sitakuangusha, naomba Mungu anisaidie kutekeleza majukumu haya.”

Mahakama Kuu Nchini Kenya iliondoa amri iliyokuwa imewekwa ya kuzuia kuapishwa kwa Prof. Kindiki kama Naibu rais wa Kenya ambapo Mkuu wa Watumishi wa umma, Felix Kosgei aliunda kamati ya watu 23 iliyopewa jukumu la kutayarisha sherehe ya kuapishwa Kiongozi huyo.

Hata hivyo, kesi ya Gachagua kupinga kuondolewa ofisini itasikilizwa kuanzia siku ya Alhamisi Novemba 7, 2024  na aliambiwa kuwa ana haki ya kukata rufaa kuhusiana na hatua iliyoamriwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii