Waandaaji wa tuzo za Grammy kupitia Recording Academy R&B Screening Committee wameiondoa album ya Tyla kwenye kipengele cha R&B na sasa imewekwa kwenye kipengele cha Muziki wa Pop licha ya kuwa na maadhi ya Muziki wa Afro-Beat, Amapiano na R&B
Jambo hilo limewashagaza watu wengi kwa sababu ya uwepo wa kipengele cha Best Progressive R&B Album kipengele maalumu ambacho kiliandaliwa kwa ajili ya kuzitambua album za pili za R&B ambazo zinakua zimejumuisha aina mbalimbali za Muziki
Watu wengi wana amini ingepaswa kuangukia hapo na sio kuondolewa kabisa na kwenda kwenye kipengele cha Pop
Mwaka 2020 Lizzo alishinda kwenye kipengele cha BEST PROGRESSIVE R&B ALBUM ambayo zamani ilifahamika kama BEST URBAN CONTEMPORARY ALBUM na album yake ambayo ilishinda inaitwa COZ I LOVE YOU
Album hiyo ilikua ya Pop lakini ndani yake ilihusisha vionjo na aina mbalimbali za muziki kama za Muziki wa R&B,Dance na Rap
Utata kama huo pia umeibuka kwa Tommy Rich Man's kupitia wimbo wake wa Million Dollar Baby kuwekwa kwenye kipengele cha Rap ukizingatia kwenye wimbo huo Tommy anaimba.. Lakini pia kwenye baadhi ya mahojiano yake amekua anakiri kuwa yeye sio msanii wa Hip-Hop
Nominees wa tuzo za Grammy watatangazwa November 8 mwaka huu na mwisho wa kupiga kura itakua ni December 12 - January 3. Lakini tuzo zitafanyika mwezi wa pili mwakani tarehe 2 huko Crypto Arena Los Angeles
So kama itafanikiwa kuwa Nominated basi yawezekana ikawa kwenye kipengele kimoja na album hizi ...
1- THE TORTURED POETS DEPARTMENT-TAYLOR SWIFT
2- HIT ME HARD & SOFT - BILLIE EILISH
3- SHORT N' SWEET - SABRINA CARPENTER
4- ETERNAL SUNSHINE - ARINA GRANDE
5- THE FALL AND RISE OF A MIDWEST PRINCESS - CHAPPELL ROANS
Cc;✍️ @baritone_tz