Waziri wa Mambo ya Nje na Ushorikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amesema kuwa ziara ya kitaifa ya siku mbili ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Cuba iliyopangwa kufanyika Novemba 6 hadi 8, 2024, imesogezwa mbele.
Balozi Kombo amesema ziara hiyo imesogezwa mbele kutokana na kuchafuka kwa hali ya hewa na dhoruba inayoitwa Rafael kupiga katika visiwa vya Cuba na mji wa Havana hivyo kusababisha ndege kushindwa kutua.
“Kiwanja cha Jose Mart kimefungwa kwa saa zaidi ya 48, hata hivyo kimbunga hicho kimeshapita na shughuli zimeanza kurejea katika hali yake ya kawaida, ziara ya Rais Samia ifanyika siku za usoni na itatolewa taarifa maalumu,” amesema Balozi Kombo
Aidha amesema kuhusu tamasha la kiswahili duniani, Rais Samia ameagiza liendelee kama kawaida likiongozwa na mawaziri waliokwenda nchini humo.