Akimbia umbali wa kilomita 160 kumuona mchumba

Mwanaume mmoja huko San Diego aliyefahamika kwa jina la Aron Greene (26) ametengeneza rekodi ya kipekee na hii ni baada ya kukimbia kilomita 160 kwa ajili ya kwenda kumuona mchumba wake.

Unaposema kilomita 160 kwa wale ambao wanasafiri mara kwa mara watakuwa mashuhuda juu ya umbali huu, lakini kwa faida ya wengi huu ni umbali kutoka Dar es salaam mpaka Mikese ambayo ni Morogoro.


''Nilikuwa nimesimama kwenye makutano ya barabara kubwa nikasema nadhani naweza kufika kwake kwa kukimbia tu'' alisema Aron Greene ambaye alikuwa anatoka San Diego kuelekea Los Angel alipo mpenzi wake, jambo ambalo lilimchukua takribani saa 32 yaani siku moja na saa 8.


Kama ulihisi huo ndiyo unaweza kuwa ukomo wa Greene basi fahamu kuwa ''Kwa wakati mwingine ningependa kuongeza umbali zaidi na kukimbia hadi John Muir trail'' alisema Greene, hii John Muir trail iko umbali wa miles 211 ambayo ni sawa na kilomita 339, umbali wa Dar es salaam mpaka Tanga

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii