Palestina Yaomba FIFA Kuifungia Israel Kujihusisha Katika Mchezo

Shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA), limetangaza wazi mpango wake wa kushughulikia ombi liliwakilishwa na Palestina kuifungia Israel kujihusisha katika mchezo wa mpira wa miguu duniani kufuatia ukiukwaji wa sheria za FIFA na vitendo vya kiubaguzi.

FIFA kupitia Rais wake, Bwana Gianni Infantino hapo jana katika kikao kilichofanyika yalipo makao makuu ya shirikisho hilo, Zurich, nchini Uswisi iliweka wazi kwamba itaanzisha uchunguzi rasmi ili kujiridhisha na mashitaka hayo kabla ya kutoa uamuzi.

“Baraza la FIFA limetekeleza uangalizi wa kina juu ya jambo hili nyeti sana, na, kulingana na tathmini ya kina, tumefuata ushauri wa wataalam huru. Vurugu zinazoendelea katika eneo hilo zinathibitisha kwamba, zaidi ya mazingatio yoye, na kama ilivyoelezwa kwenye kongamano la 74 la FIFA, tunahitaji amani.

“Huku tukiendelea kushtushwa sana na kinachoendelea.” alisema Gianni Infantino

kufuatia uamuzi uliofanyika katika kikao hicho cha hapo jana Alhamisi tarehe 3 Oktoba 2024 ambae pia aliambatisha na salamu za pole na kuziomba nchi hizo zitafute namna ya kurudisha amani.

Kwa madai ya shirikisho la mpira wa miguu Palestine, (PFA) limeishitaki shirikisho la mpira wa miguu Israel, (IFA) kwa ‘ukiukaji wa sheria za kimataifa kupitia kukalia kwa mabavu Ukanda wa Gaza, Ubaguzi dhidi ya wanamichezo wa Kipalestina katika vilabu viwili vya Israeli na ukiukaji wa sheria za FIFA kupitia ushiriki wa ligi ya vilabu vitano vya Israeli kutoka kwa makazi haramu kwenye ardhi ya Palestina.’

Hata hivyo, madai hayo yamekataliwa moja kwa moja na Israel kwa kukanusha taarifa hizo sio za kweli huku FIFA ikiendelea na uchunguzi kabla ya kutoa maamuzi kamili.

Nchi zote hizo mbili timu zake za taifa za wanaume zitacheza katika wiki inayofuata, Palestine itacheza na Iraq katika mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu kombe la dunia mwaka 2026 mchezo unaotarajiwa kuchezwa tarehe 10 Oktoba, huku Israel ikitarajiwa kucheza mchezo wa UEFA Nations League dhidi ya Ufaransa siku hio hio.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii