Benki kuu ya Tanzania (BoT) imeendesha mafunzo maalum kwa
waandishi wa habari kutoka mikoa ya Magharibi kwa lengo la kuwajengea uwezo wa
kuelewa na kutafsiri kwa usahihi majukumu na kazi za benki hiyo katika uchumi
wa taifa.
Mafunzo hayo ya siku mbili ambayo yameanza
Mkoani Kigoma yamehusisha mikoa ya Kigoma, Katavi, Kagera na Tabora lengo
likiwa ni kuwawezesha wanahabari hao kuchambua na kuandaa habari kuhusu masuala
ya fedha na uchumi kwa ufasaha.
Awali akifungua mafunzo hayo, Meneja msaidizi wa Uhusiano wa umma, Benki kuu ya Tanzania (BoT) Bi. Noves Moses AMEZUNGUMZA KUHUSU LENGO LA SEMENA HIYO NA amewataka wanahabari hao kutumia vyema mafunzo hayo kutoa elimu kwa jamii kupitia vyombo vya habari.
Kupitia mafunzo hayo mada mbalimbali zinatarajiwa kuwasilishwa ikiwemo namna BoT inavyosimamia mifumo ya malipo nchini, muundo na majukumu ya Benki hiyo ambapo imeelezwa kuwa jukumu lake la msingi ni kuandaa na kutekeleza sera ya fedha nchini kwa lengo a kudhibiti mfumko holela wa bei na kuhakikisha utulivu wa uchumi nchini unakuwepo.
Hata hivyo Aisha amesema kuwa wanatarajia kuona jamii ikipata uelewa juu ya huduma ndogo ndogo za fedha na utambuzi wa alama kwenye noti.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime