Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mhe. Amiry Mkalipa amesema serikali haitolipa fidia kwa wananchi waliovamia eneo la kingo za mto Msuka huku akiwataka wananchi kutoendesha shughuli za kilimo kando ya mto huo.
Amebainisha hayo LEO akiwa katika kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya Utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Kwa kipindi Cha kuanzia Julai Hadi Desemba 2026, Mkutano uliohusisha Wajumbe mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Kafiti William Kafiti.
Katika Kikao hicho, Mhe. Mkalipa amesema wananchi wanaondesha shughuli za kilimo kando ya mto huo wanasababisha uharibifu wa kingo za mto hali inayopelekea maji kusambaa kwenye makazi ya watu.
Katika hatua nyingine Mkalipa amewataka wananchi wanaofanyabiashara katika maeneo yasiyoruhusiwa ikiwemo miundombinu ya umeme kuacha kufanya hivyo ili kulinda usalama wao.
Kwa Upande wake Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Kafiti William Kafiti ameitaka halimashauri kutumia mitambo yake kufanya matengenezo ya barabara zote korofi huku akitaka kutengwa kwa eneo maalumu la uchimbaji wa moramu za ukarabati huo.
Maelekezo hayo yanajiri kufuatia malalamiko ya madiwani na viongozi wa serikali za mitaa yaliyowasilishwa katika kikao hicho ikiwemo ubovu wa barabara, Maji, Umeme, Afya na ulinzi.
Sasa ili kupata undani wa taarifa hii tafadhali usikose kutufuatilie na Usikilize jembe Habari Kamili hapo saa kumi kamili jioni ambapo msomaji wetu wa hii leo ni Jacob Richard Mlay tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa. Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz #10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime