Isak anatarajiwa kurejea Uwanjani hivi karibuni

Kocha mkuu wa Liverpool, Arne Slot, ametoa habari njema kwa mashabiki wa klabu hiyo baada ya kuthibitisha rasmi muda wa kurejea kwa mshambuliaji wao hatari, Alexander Isak.

Akizungumza na waandishi wa habari, Slot ameweka wazi kuwa mchakato wa kupona kwa nyota huyo unakwenda vyema na sasa anatarajiwa kuungana na kikosi cha kwanza kuanzia mwishoni mwa mwezi Machi au mapema mwezi Aprili ingawa pamoja na habari hiyo ya matumaini, Slot amewataka mashabiki kuwa na subira kidogo kwani Isak atahitaji muda wa kupata kuwa sawa uwanjani kabla ya kuanza kutikisa nyavu kama ilivyozoeleka.

 "Tunatarajia kumuona mchezaji tofauti kabisa kuelekea mwishoni mwa msimu huu kuliko tulivyomuona mwanzoni. Lakini, ni lazima afahamu kuwa atahitaji muda kidogo ili kurudi kwenye kasi yake ya kawaida. Kusema kweli, bado hatujamuona Alex bora zaidi mpaka sasa," alisema Slot kwa kujiamini.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii