Venezuela: Rais Maduro atishia kuwafunga viongozi wa upinzani

Wakati akiendelea kupata shinikizo la kimataifa kuhalalisha kuchaguliwa kwake tena, rais wa Venezuela Nicolas Maduro ametishia hivi punde siku ya Jumatano Julai 31 kuwafunga viongozi wawili wa upinzani, Maria Corina Machado na Edmundo Gonzalez Urrutia, akiapa kwamba wapinzani wake hawatafikia "kamwe madaraka".

Mrithi wa kiongozi wa kisoshalisti na mtetezi wa sera ya Hugo Chávez, Nicolás Maduro, 61, aliye madarakani tangu mwaka 2013, alitangazwa kuchaguliwa tena kwa muhula wa tatu hadi mwaka 2031, kufuatia kura za Jumapili baada ya kushinda kwa 51.2% ya kura dhidi ya 44.2% ya mpinzani wake Edmundo Gonzalez Urrutia, kulingana na matokeo rasmi. Matokeo yanayopingwa na nchi nyingi, wakati upinzani unaendelea kuandamana kupinga matokeo ya uchaguzi na ushindi wa Nicolas Maduro, lakini unakabiliwa na ukandamizaji kutoka kwa serikali.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii