Ruben Amorim anatajwa kuwa Kocha mpya Man United

Kocha huyo anayefundisha Sporting Lisbon ambayo ni Mabingwa watetezi wa ligi ya Ureno na ndiyo vinara wa ligi hiyo msimu huu wa 20245-2025 ikiwa na alama 27, katika michezo tisa ikifunga goli 30 na kuruhusu goli mbili . 


Kocha wa klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno Ruben Amorim kwa mujibu wa vyombo vya Habari barani Ulaya vinamtaja kuwa ndiye kocha anayetizamiwa kuchukua nafasi ya Erik Ten Hag ndani ya Manchester United baada ya timu hiyo kutangaza kumfuta kazi Kocha huyo raia wa Uholanzi siku ya jana. Klabu ya Man United na Sporting Lisbon zipo kwenye majadiliano juu ya uhamisho wa Kocha huyo bora kwa sasa nchini Ureno.

Amorim raia wa Ureno amekiongoza kikosi cha Mbingwa watetezi wa ligi kuu ya Ureno tangu Machi 2020,amekifanikisha kikosi hiko kushinda ubingwa wa Primeira Liga mara mbili mtawalia na kwa mara ya kwanza msimu wa 2020-21 baada ya kupita miaka 19 bila kushinda taji hilo na msimu wa 2023-24 ikwa mara ya pili ndani ya miaka mitatu kushinda ubingwa huo. 

Sababu kubwa inayotizamwa na Mabosi wa Manchester United kufikiria kumpatia majukumu ya kuinoa timu hiyo inayotumia uwanja wa Old Trafford ni ubora wake wa kujenga timu kwa kutumia bajeti ndogo, huku akisifika pia kwa kubadilisha na kupandisha viwango vya Wachezaji na kuwafanya kuwa bora. United inawachezaji wengi Wazuri wanaohitaji Kocha kuwapeleka hatua nyingine kiuchezaji hilo ni swali ambalo majibu yake yapo kwenye kichwa cha Mtaalamu huyo kutoka Ureno.

Nyota huyo wa zamani wa Benfica anasifika kwa kupenda kucheza soka la kushambulia na kupeleka mkandamizo kwa Wapinzani kwa haraka ili kuupoka mpira tena na kuurudisha kwenye himaya yao. Viongozi wa Mashetani Wekundu wanahitaji Mwalimu ambaye anafalsafa ambayo itwenda kubadili namna timu hiyo inavyocheza ili kurudisha heshima ya klabu kwa kushinda nataji na furaha kwa Mashabiki wa Man U Duniani kote.

Amorim anatizamwa kama mmoja wa Makocha vijana wenye uwezo mkubwa kimbinu na kujenga timu shindani pia uzoefu wake wa kushinda mataji katikati ya timu mbili Benfica na FC Porto  ambazo zimekuwa zikitawala ligi ya Ureno ni sababu moja wapo inayomfanya awe mbele ya wengine kwenye kuwania nafasi ya kufundisha United.

Wakufunzi kutoka Ureno wanafanya kazi nzuri  kwenye ligi ya Uingereza Marco Silva wa Fulham, Nuno Espirito Santos, wanafanya kazi kubwa kwenye timu zao kumekuwa na urahisi wa kuzoea ligi ya Uingereza kwa Makocha kutoka Ureno kuliko kutoka mataifa mengine. Jose Mourinho mfano mkubwa alitoka Ureno akiwa Kocha wa FC Porto akaiongoza Chelsea msimu wake wa kwanza kwa rekodi ya kuchukua ubingwa na kuruhusu kufungwa goli 15 katika michezo 38 ya ligi.

Kocha huyo anayefundisha Sporting Lisbon ambayo ni Mabingwa watetezi wa ligi ya Ureno na ndiyo vinara wa ligi hiyo msimu huu wa 20245-2025 ikiwa na alama 27, katika michezo tisa ikifunga goli 30 na kuruhusu goli mbili .

Manchester United inahitaji kuanza upya kwa kuamini kwenye Kocha kijana ambaye anauwezo wa kujenga timu yenye kubeba taswira ya falsafa yake. Arsenal imenufaika kwa Kocha kijana Mikel Arteta amefanikiwa kukibadili kikosi cha Washika mitutu wa London, kama Man U itampata Ruben Amorim na wakampatia uhuru wa kujenga timu na wakamvumilia anaweza akawa Mwalimu sahihi kuirudisha klabu hiyo kwenye njia ya mafanikio ambayo yatakuwa endelevu ndani ya klabu hiyo tanga Sir Alex Ferguson afanikiwe kufanya hivyo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii